Hukumu ya Swalah ya Ijumaa Swalah ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu, aliyebaleghe, asiye na udhuru wa kuiacha.
Dalili ya hilo:
Neno la Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Kukinadiwa Swala kwa siku ya Ijumaa, endeni kwa haraka kwenye utajo wa Mwenyezi Mungu, na muache biashara} [62: 9].
Neno la Mtume ﷺ: ( Hawatoacha watu kuhudhuria Ijumaa, au Mwenyezi Mungu Atapiga mihuri juu ya nyoyo zao, kisha wawe ni miongoni wa walioghafilika) [Imepokewa na Muslim]. https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-ijumaa